Asubuhi ya j5 ya leo Nov 14….mtu
mzima Saigon amegonga interviews mbili ambazo kila moja amejaribu kuzungumzia
mambo tofauti…interview yake ya kwanza amefanya na mtandao wa ThisIs50 ambapo
ameegemea zaidi ishu yake na member wa Mobb Deep…Prodigy…interview yake ya pili
amefanya ndani ya Power 105.1.
Leo nadondoka na interview yake
ndani ya Power 105.1 coz nahisi alichozungumzia katika interview hiyo kina
mguso wa hali ya juu…rapper huyo kutoka New York amesema angekuwa na uwezo
angewachapa ngumi Rick Ross na 2 Chainz na kuwafanya mfano kwa rappers wengine
wote wenye muelekeo kama wao.
Kikubwa ambacho kimepelekea Saigon kusema
hivyo ni content (maudhui) ya muziki wa Rick Ross na 2 Chainz ambao yeye
anauona ni hatari kwa kizazi cha sasa (teenagers)…kizazi ambacho yeye anafahamu
kuwa ndo kizazi shabiki cha muziki wa HipHop na anaufananisha muziki wa rappers
hao na rappers wengine wengi wanaochipuka kama uyoga hivi sasa na wenye
muelekeo huo na movie za ngono.
“Iko nje ya uwezo wangu…lakini
unafahamu..??ningekuwa na uwezo ningewachapa ngumi kama wasipobadili jumbe za
nyimbo zao…ningependa kuwachapa ngumi kila mmoja…Rozay, 2 Chainz na yeyote
anayetengeneza muziki unaoharibu watoto wetu…mi nashangaa…hawa wote
wanalitegemea soko hili la hawa watoto…sote tunafahamu kuwa hata ukienda
kununua movie za ngono…kuna utaratibu wake ki-umri…so inakuwaje unaimba
visivyostahili kwa watoto na soko lako ni hao watoto..??sitaki kutengeneza
battle na watoto wangu mwenyewe ambao wamekuwa influenced na muziki wao…nina
watoto mimi ujue..??Kuna siku nilikuwa kwenye 106 & Pack…nilihuzunika sana
kuona mabinti wadogo wenye miaka 13 au 14 wanafuatisha lyrics zenye maneno
yanayozungumzia malaya wanavyofanya ngono…nikashtuka sana…nikawaza nani
alaumiwe kwa hili..”?..amesema Saigon.
Akaongeza..”siwataji Rick Ross, 2
Chainz na wengineo pekee…bali ni mtu yeyote anayehusika na hilo…wote lao
moja…kwangu mimi maendeleo ya rap ni kutafuta kinachoipandisha na kuishusha
pia”.
No comments:
Post a Comment