Friday, October 26, 2012

Janet Jackson afuata nyayo za Michael Jackson, abadili dini kimyakimya na kuwa Muislam.

Mshindi wa tuzo za grammy mara tano Janet Jackson ambae pia ni mdogo wake Marehemu Michael Jackson, ni kama anafuata nyayo za kaka yake hata katika maswala ya imani.
Kwa mujibu wa muandishi mashuhuri wa Uturuki, Adam Oktar, Janet Jackson amebadili dini na kuwa muislam kimyakimya na ameamua kuwaficha fans wake katika hili.
Taarifa hii imekuja wakati Janet Jackson anasubiri kufunga ndoa na millionaire wa Qatar ambae ni mchumba wake wa sasa Wissam Al Mana. Na taarifa zinasema kuwa wawili hao wanatarajia kufunga ndoa huko Doha Qatar mapema mwaka kesho kwa kufuata imani na misingi ya Kiislam.
Chanzo kimoja kimesema wawili hao wanatarajia kutumia mkwanja kiasi cha dola za kimarekani million 3 kuzungukia kwa ndege wageni watakaohudhuria takribani 500, na kila mgeni atapewa zawadi ya kuonesha kumbukumbu ya ndoa hiyo na shukurani kwa kufika katika sherehe hiyo, zawadi hiyo inatarajiwa kuwa saa ya mkononi yenye thamani ya dola za kimarekani 10,000….ambazo ni kama fedha za kibongo zaidi ya million 15 kwa hiyo saa moja.
Kwa hali hiyo inaonesha kabisa kuwa wageni hao wataikumbuka sana ndoa hiyo ya mwanadada Janet Jackson na Millionaire wa Qatar Wissam Al Mana.

No comments:

Post a Comment